Hakika Mola wako Mlezi humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika Mola wako nawakunjulia riziki baadhi ya watu na Anawabania wengine kulingana na ujuzi Wake na hekima Yake, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake. Yeye Ndiye Mwenye kuyaona mambo ya ndani ya waja Wake, hakuna chochote katika hali zao kilicho nje ya ujuzi Wake.